Nafasi ya kazi: Mratibu - Shirika la Wakulima Wetu Tarime (WAWETA)

Shirika la Wakulima Wetu Tarime (WAWETA) ni shirika lisilokuwa la kiserikali lililo anzishwa mwaka 2014 na kusajiriwa chini ya sheria ya usajiri mashirika Na. 24 kifungu 12 (2) ya mwaka 2002 na kupata Namba OONGO/08208 likiwa na lengo la kuwajengea uwezo Wakulima na Wafugaji kwa kutoa elimu ya Kilimo na ufugaji wenye tija na endelevu.

Kutokana na mikakati ya Shirika ya mwaka 2017, Shirika linahitaji kuajiri nafasi moja (1) ya MRATIBU wa SHIRIKA ambaye atasimamia shughuli za shirika Wilayani Tarime kwa kushirikiana na Bodi ya Shirika WAWETA ili kufikia malengo iliyojipangia.

SIFA ZA MUOMBAJI: 

1) Awe Mtanzania mwenye akili timamu, 
2) Asiwe na historia ya kushitakiwa kwa makosa ya jinai, 
3) Awe na umri kati ya miaka 22 hadi 45, 
4) Awe na elimu ya kidato cha IV na kuendelea 
5) Awe na cheti cha stashahada (Diploma) ya Kilimo na mifugo kutoka chuo kinacho tambuliwa na serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Kama atakuwa amepata elimu nje ya nchi ni lazima aambatanishe cheti kilicho thibitishwa na baraza la vyuo na ufundi (NACTE). 
6) Awe na uwezo wa kufanya kazi na vikundi vya Wakulima. 
7) Awe na leseni ya kuendesha chombo cha moto hususani pikipiki. 

JINSI YA KUOMBA

Barua ya maombi iliyoambatanishwa na nakala za vyeti vya elimu, kitambulisho cha mpiga kura, cheti cha kuzaliwa , na au barua ya uthibitisho kutoka ofisi ya mtaa au kitongoji, namba ya simu pamoja na barua pepe ya muombaji yatumwe kwa barua pepe: 

waweta.tarime@yahoo.com

AU 

Anuani Ifuatayo: 
MWENYEKITI SHIRIKA LA WAKULIMA WETU TARIME (WAWETA) 
S.L.P. 16 TARIME 

Pia maombi yanaweza kuletwa ofisi ya WAWETA MAKAO MAKUU ofisi iko jirani na ofisi ya idara ya Kilimo Halmashauri ya wilaya ya Tarime au ofisi ya idara ya Kilimo kuanzia saa 1.30 hadi saa 9.30 alasiri siku zote mpaka tarehe ya mwisho 30/01/2017 

Kwa mawasiliano simu namba: 0764218172, 0753193715 

NB: MUOMBAJI ATAJIGHARAMIA USAFIRI NA FEDHA ZA KUJIKIMU

*MWISHO wa kutuma maombi haya ni tarehe 30/01/2017 saa 9.00 Alasiri, na Usaili kwa wote waliotuma maombi utafanyika tarehe 31/01/2017 kuanzia saa 3.00 Asubuhi katika ofisi ya WAWETA iliyopo jirani na Ofisi ya kilimo , Halmashauri ya Wilaya Tarime.


Tembelea Job Site Tz kwa nafasi za kazi na ajira zaidi


Labels: