Maelezo ya Shirika
Shirika la Wakulima Wetu Tarime (WAWETA) ni shirika lisilokuwa la kiserikali lililo
anzishwa mwaka 2014 na kusajiriwa chini ya sheria ya usajiri mashirika Na. 24
kifungu 12 (2) ya mwaka 2002 na kupata Namba OONGO/08208 likiwa na lengo la
kuwajengea uwezo Wakulima na Wafugaji kwa kutoa elimu ya Kilimo na ufugaji
wenye tija na endelevu.
Kutokana na mikakati ya Shirika ya mwaka 2017 Shirika linahitaji kuajiri nafasi
moja (1) ya Afisa Kilimo Msaidizi (Agricultural Field Officer) ambaye atafanya
shughuli za shirika Mfano kutoa mafunzo kwa wakulima Wilayani Tarime, kutoa
elimu ya mifugo kwa wakulima kwa kushirikiana na Mratibu, Bodi ya Shirika
WAWETA ili kufikia malengo iliyojipangia.
Sifa za muombaji
1) Awe Mtanzania mwenye akili timamu,
2) Asiwe na historia ya kushitakiwa kwa makosa ya jinai,
3) Awe na elimu ya kidato cha IV na kuendelea
4) Awe na elimu ngazi ya cheti(certificate) au stashahada (Diploma) ya Kilimo na
mifugo (General Agriculture) kutoka chuo kinacho tambuliwa na serikali ya
Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Kama atakuwa amepata elimu nje ya nchi ni
lazima aambatanishe cheti kilicho thibitishwa na baraza la vyuo na ufundi
(NACTE).
5) Awe na uwezo wa kufanya kazi na vikundi vya Wakulima.
6) Awe na leseni ya kuendesha chombo cha moto hususani pikipiki.
Namna ya kutuma maombi
Barua ya maombi iliyoambatanishwa na nakala za vyeti vya elimu, kitambulisho
cha mpiga kura, na au barua ya uthibitisho kutoka ofisi ya mtaa au kitongoji,
namba ya simu pamoja na barua pepe ya muombaji yatumwe kwa barua pepe waweta.tarime@yahoo.com
Au anuani ifuatayo:
MWENYEKITI,
SHIRIKA LA WAKULIMA WETU TARIME,
S.L.P. 16,
TARIME
Pia maombi yanaweza kuletwa ofisi ya WAWETA MAKAO MAKUU ofisi iko jirani
na ofisi ya idara ya Kilimo Halmashauri ya wilaya ya Tarime au ofisi ya idara ya
Kilimo kuanzia saa 1.30 hadi saa 9.30 alasiri siku zote jumatatu hadi jumamosi, tarehe ya mwisho kutuma maombi 11/02/2017.
Kwa mawasiliano simu
namba: 0764218172, 0753193715
NB: MUOMBAJI ATAJIGHARAMIA USAFIRI NA FEDHA ZA KUJIKIMU.
Labels: NAFASI ZA KAZI