Afisa Kilimo Msaidizi - WAWETA

Afisa-kilimo-msaidizi-waweta

Maelezo ya Shirika

Shirika la Wakulima Wetu Tarime (WAWETA) ni shirika lisilokuwa la kiserikali lililo anzishwa mwaka 2014 na kusajiriwa chini ya sheria ya usajiri mashirika Na. 24 kifungu 12 (2) ya mwaka 2002 na kupata Namba OONGO/08208 likiwa na lengo la kuwajengea uwezo Wakulima na Wafugaji kwa kutoa elimu ya Kilimo na ufugaji wenye tija na endelevu.

Kutokana na mikakati ya Shirika ya mwaka 2017 Shirika linahitaji kuajiri nafasi moja (1) ya Afisa Kilimo Msaidizi (Agricultural Field Officer) ambaye atafanya shughuli za shirika Mfano kutoa mafunzo kwa wakulima Wilayani Tarime, kutoa elimu ya mifugo kwa wakulima kwa kushirikiana na Mratibu, Bodi ya Shirika WAWETA ili kufikia malengo iliyojipangia.

Sifa za muombaji

1) Awe Mtanzania mwenye akili timamu, 
2) Asiwe na historia ya kushitakiwa kwa makosa ya jinai, 
3) Awe na elimu ya kidato cha IV na kuendelea 
4) Awe na elimu ngazi ya cheti(certificate) au stashahada (Diploma) ya Kilimo na mifugo (General Agriculture) kutoka chuo kinacho tambuliwa na serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Kama atakuwa amepata elimu nje ya nchi ni lazima aambatanishe cheti kilicho thibitishwa na baraza la vyuo na ufundi (NACTE). 
5) Awe na uwezo wa kufanya kazi na vikundi vya Wakulima. 
6) Awe na leseni ya kuendesha chombo cha moto hususani pikipiki. 

Namna ya kutuma maombi

Barua ya maombi iliyoambatanishwa na nakala za vyeti vya elimu, kitambulisho cha mpiga kura, na au barua ya uthibitisho kutoka ofisi ya mtaa au kitongoji, namba ya simu pamoja na barua pepe ya muombaji yatumwe kwa barua pepe waweta.tarime@yahoo.com 

Au anuani ifuatayo: 

MWENYEKITI, 
SHIRIKA LA WAKULIMA WETU TARIME, 
S.L.P. 16, 
TARIME 

Pia maombi yanaweza kuletwa ofisi ya WAWETA MAKAO MAKUU ofisi iko jirani na ofisi ya idara ya Kilimo Halmashauri ya wilaya ya Tarime au ofisi ya idara ya Kilimo kuanzia saa 1.30 hadi saa 9.30 alasiri siku zote jumatatu hadi jumamosi, tarehe ya mwisho kutuma maombi 11/02/2017. 

Kwa mawasiliano simu namba: 0764218172, 0753193715

NB: MUOMBAJI ATAJIGHARAMIA USAFIRI NA FEDHA ZA KUJIKIMU. 
MWISHO wa kutuma maombi haya ni tarehe 11/02/2017 saa 9.00 Alasiri, Watakaofanikiwa watajulishwa kufika kwenye usaili tarehe 13/02/2017 .


 Tembelea Job Site Tz kwa nafasi za kazi na ajira zaidi


Labels: