Soya au Soybean (kwa kiingereza) ni zao la jamii ya mikunde. Kwa kitaalam linaitwa Glycine max. Zao hilo asili yake ni nchi ya China ambako lilianza kulimwa takribani miaka 4800 iliyopita. Zao la soya liliingizwa nchini Tanzania mwaka wa 1907 katika maeneo ya Amani mkoani Tanga.
1. HISTORIA,
UMUHIMU NA AINA ZA SOYA
Historia
ya zao la Soya nchini Tanzania
Soya au Soybean (kwa kiingereza) ni zao la jamii ya mikunde. Kwa kitaalam linaitwa Glycine
max.
Zao hilo asili yake ni nchi ya China
ambako lilianza kulimwa takribani miaka 4800 iliyopita. Zao la soya liliingizwa
nchini Tanzania mwaka wa 1907 katika maeneo ya Amani mkoani Tanga. Kati ya
miaka ya 1930 na 1960, kilimo cha soya kilipanuka na kuenea hadi maeneo ya
Nachingwea mkoa wa Mtwara, Kilosa mkoa wa Morogoro na Peramiho mkoa wa Ruvuma.
Kuenea kwa zao hilo katika maeneo hayo kulitokana na msukumo wa mashirika ya Overseas
Food Co-operation – (OFC), State Trading Cooperation (STC), General
Agricultural Production for Export – (GAPEX) na National Milling Corporation
– (NMC). Mashirika hayo yalisafi risha soya kwenda katika nchi za Japan na
Singapore. Kwa kuwa uzalishaji wa zao hilo katika mikoa hiyo ulilenga soko la
nje, wananchi hawakufundishwa matumizi yake na kwa sababu hiyo baada ya
mashirika hayo kuacha biashara ya zao hilo kilimo cha soya kilifi fi a hadi mwishoni
mwa miaka ya 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990 ambapo uzalishaji ulianza tena
baada ya jamii kuhamasika katika matumizi ya soya hasa katika kutengeneza
vyakula vya watoto.
Umuhimu
wa zao la Soya
|
Soya iliyokomaa |
Soya ni
zao lenye virutubisho vingi vya aina ya protini ikilinganishwa na virutubisho
vya aina hiyo katika mazao mengine ya mimea na hata katika baadhi ya vyakula
vinavyotokana na wanyama kama nyama na mayai na maziwa. Sifa hizo za soya
zinafanya zao hilo, kuwa na umuhimu wa kipekee katika kutengeneza vyakula vya
binadamu na mifugo na matumizi katika viwanda vya madawa na matumizi mengineyo.
Mafuta yatokanayo na soya hayana lehemu (cholesterol) na hivyo kuwa na
sifa ya kuboresha afya ya walaji.
Zifuatazo
ni faida za kutumia soya:-
(i.) Soya
ina virutubisho vingi na vilivyokamilika vya aina ya protini ambayo ni muhimu
katika kuboresha lishe na afya kwa binadamu na mifugo;
(ii.) Soya
ni chanzo rahisi na chenye gharama nafuu cha protini ambacho hata mtu wa kipato
cha chini anaweza kumudu kwa kuwa zao hilo linaweza kulimwa maeneo mengi hapa
nchini;
(iii). Kwa
kuwa soya ina kiasi kikubwa cha protini ikilinganishwa na nyama na mayai na
maziwa, inasaidia kupunguza kasi ya mashambulizi ya vijidudu vya maradhi
mbalimbali ikiwa ni pamoja na magonjwa ya kansa, moyo, na kuwaongezea nguvu
wagonjwa hasa wa UKIMWI;
(iv.) Soya
ni zao muhimu kwa watu wa kipato cha chini katika kuondoa utapiamlo hususani
kwa watoto kwa kuwa hawawezi kumudu gharama za vyanzo vingine vya protini kama
nyama na mayai;
(v.)
Kutokana na uwingi wa protini, matumizi ya soya kwa watoto yanasaidia viungo
kukua kwa haraka;
(vi.) Soya
hurutubisha udongo kwa kutumia njia ya nitrogen fixation. Kwa hiyo ni
zao linalofaa kutumika katika kilimo cha mzunguko (crop rotation)
na katika kurutubisha ardhi ;
(vii.) Soya
huongeza kipato na ni zao linaloweza kuchangia katika kuondoa umaskini kwa
mkulima kutokana na gharama ndogo za uzalishaji. Aidha, ni zao linaloweza
kuondoa umaskini kwa watengenezaji wa vyakula vya binadamu na mifugo,
wafanyabiashara na wafugaji na kutoa ajira kwa rika zote yaani vijana na wazee,
vijijini na mijini; na
(viii.)
Utafi ti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa mafuta ya soya yanaweza kutumika kwa
kuendeshea mitambo yaani bio-fuel na bio-diesel.
Aina
za Soya
Kuna aina
mbalimbali za soya, aina zilizozoeleka Tanzania na pamoja na:
Bossier,
Uyole soya 1, Ezumu Tumu, Delma Hermon, Duiker na
Kaleya.
Kila aina
inahitaji mazingira na hali ya hewa inakowezakustawi, kukomaa kwa muda maalum
na kutoa mavuno mazuri. Hata hivyo Bossier ni aina ambayo hustawi katika maeneo
mengi nchini. Kwa wastani, aina mbalimbali za soya huchukua wastani wa miezi
mitatu hadi saba kukomaa kutegemea na aina, mahali ilikopandwa na utunzaji
katika shamba.
2. MAZINGIRA,
MVUA NA RUTUBA YA UDONGO
Mazingira
na mikoa inayofaa kilimo cha soya
|
Mmea wa soya uliozaa |
Soya
inaweza kulimwa katika sehemu zote zenye sifa na zinazofaa kwa kilimo cha
maharage na mahindi. Sifa hizo ni pamoja na mvua ya kutosha, udongo
usiotuamisha maji na udongo tifutifu usio na mchanga mwingi. Kutokana na kuwepo
kwa maeneo mengi nchini yenye sifa hizo, ni dalili kuwa zao la soya linaweza
kustawi katika maeneo hayo ambayo yapo karibu nchi nzima.
Jambo
muhimu linalotakiwa ni kufahamu na kupanda aina za soya zinazofaa katika eneo
husika kulingana na maelekezo ya wataalamu. Kwa sasa mikoa inayoongoza kwa
kilimo cha soya ni Ruvuma, Mbeya, Rukwa, Iringa na Morogoro. Mikoa mingine
yenye uwezo na sifa za kuzalisha soya ni Tanga, Mtwara, Lindi, Kagera, Mara,
Kigoma, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
Kwa mujibu
wa tathmini iliyofanywa na Wizara ya Kilimo na Chakula mwaka wa 2005, zaidi ya
tani milioni mbili za soya zinaweza kuzalishwa kwa mwaka endapo maeneo yote ya
nchi yanayofaa kwa kilimo cha soya yakitumika ipasavyo. Uzalishaji wa sasa
unakadiriwa kuwa tani elfu tano (5,000). Kiwango hiki cha uzalishaji
ni cha chini sana ukilinganisha na kiwango kinachoweza kufi kiwa. Aidha, kiasi
hiki kidogo na uwezo unaoweza kufi kiwa ni changamoto katika kuongeza
uzalishaji na matumizi ya zao hilo.
Mahitaji
ya Mvua
Soya
huhitaji wastani wa mililita 350 hadi 1,500 za mvua kwa mwaka na inayonyesha
kwa mtawanyiko mzuri hususan katika kipindi chote cha ukuaji wa zao hilo. Soya
pia inafaa katika kilimo cha umwagiliaji kwani katika maeneo hayo kunakuwa na
uhakika wa unyevu muda wote. Jambo la kuzingatia ni kutowepo kwa mvua wakati
soya inapokauka.
Rutuba
ya Udongo na Mahitaji ya Mbolea
|
Mmea wa soya kabla haujazaa |
Kama
ilivyo kwa mazao mengi, soya pia huhitaji udongo wenye rutuba na usiotuamisha
maji. Hivyo endapo soya italimwa katika sehemu yenye rutuba hafi fu, itahitaji
mbolea kama mazao mengine ijapokuwa huvumilia udongo wenye rutuba hafi fu. Kwa
hiyo uamuzi wa kutumia au kutotumia mbolea na kiwango cha kutumia utategemea
rutuba iliyopo kwenye udongo katika eneo husika. Hata hivyo, soya huhitaji wastani
wa kilo 80 hadi 100 za mbolea aina ya DAP na TSP kwa hekta moja na kilo 60 hadi
80 kwa mbolea aina ya CAN kwa hekta moja. Mtaalamu aliyepo karibu na mkulima
anaweza kushauri hali ya rutuba ya udongo katika eneo husika. Jambo la
kuzingatia wakati wa kupanda ni kuhakikisha kuwa mbolea haigusani na mbegu kwa
sababu mbolea itaunguza mbegu na hazitaota. Samadi iliyoiva pamoja na mbolea
nyingine za asili pia zinafaa kutumika katika kilimo cha soya.
3. UTAYARISHAJI
NA UTUNZAJI WA SHAMBA LA SOYA
Kutayarisha
shamba
Shamba la
soya linahitaji maandalizi mazuri kama ilivyo kwa mazao mengine. Utayarishaji
huo wa shamba ni pamoja na kuondoa magugu yote kwa kuwa soya haivumilii magugu
hasa ikiwa katika hatua za mwanzo za ukuaji (seedling stage).
Shamba la
soya linaweza kulimwa kwa sesa au matuta. Kilimo cha sesa chaweza
kulimwa kwa kutumia jembe la mkono au la kukokotwa na wanyama kazi kama maksai
na punda au kwa kutumia trekta. Kilimo cha matuta kukinga mteremko kinafaa na
kinapendekezwa kwa maeneo yenye mwinuko. Vilevile kilimo
cha matuta kinafaa sehemu tambarale lakini zenye mvua nyingi ili kupunguza
madhara ya maji yanayotuama baada ya mvua kubwa kunyesha.
Mbegu
Ni muhimu
kuandaa mbegu bora na safi mapema kabla ya msimu wa mvua kuanza. Kwa
wastani kilo 20 hadi 30 za mbegu za soya zinatosha kwa hekta moja
kutegemeana na aina ya mbegu. Kwa kuwa aina nyingi za soya hazistawi
kila mahali, ni muhimu kwa mkulima kuhakikisha kuwa anatumia mbegu
inayofaa katika eneo analotaka kulima soya hususani mahitaji ya mvua. Kwa
sababu hiyo ni muhimu kwa mkulima kupata ushauri toka kwa mtaalam aliyekaribu
naye kabla ya kuamua kulima soya. Aidha, mkulima anashauriwa kununua na kutumia
mbegu kutoka katika sehemu ambazo chanzo cha mbegu hizo kinaeleweka. Mfano wa
sehemu hizo ni pamoja na maduka ya pembejeo, wakala wa mbegu, mashamba ya mbegu
na vituo vya utafi ti. Hii ni kwa sababu mbegu ya soya hupoteza nguvu ya uotaji
katika msimu mmoja hasa katika sehemu za joto. Kwa hiyo mkulima anatakiwa
kuhakikisha kuwa anapanda mbegu itakayoota. Kama mkulima hana uhakika na chanzo
cha mbegu au ana wasiwasi wa kuota kwa mbegu alizonazo anaweza kufanya majaribo
ya uotaji (germination test) kabla ya kupanda. Njia rahisi ni
kuzilowesha mbegu kwa maji na kisha kuziweka kwenye kitambaa mahali penye joto
la kutosha. Mbegu ziloweshwe na maji kila siku mpaka zitakapoota. Hesabu mbegu
zilizoota na iwapo mbegu zilizoota ni chini ya 75 kati ya mbegu 100 yaani
asilimia 75, mkulima anashauriwa kutopanda mbegu hizo.
Wakati
wa kupanda
Upandaji
wa soya unategemea na aina na mahali husika. Kwa aina za soya zinazokomaa mapema,
soya ikipandwa mwanzoni mwa msimu wa mvua katika maeneo yanayopata mvua kwa kipindi
kirefu itakomaa wakati mvua bado zinaendelea kunyesha na hivyo kufanya uvunaji
na ukaushaji kuwa mgumu na kuhitaji nguvu kazi na muda wa ziada la sivyo mbegu
zitaoza au kuanza kuota na kupoteza ubora wake. Kwa hiyo ni budi kujua mwenendo
wa mvua mahali husika ili kupanda kwa wakati na aina ya soya kulingana na
mahali hapo. Jambo la muhimu ni kuhakikisha kuwa soya inakomaa wakati hakuna
mvua ili kurahisisha uvunaji na soya kutooza. Jedwali Namba 1 linaonyesha
mahali, aina na muda wa
kupanda soya.
Jedwali
Namba 1: Muda unaoshauriwa kupanda soya
Na.
|
Mahali
|
Mbegu
|
Muda
|
1
|
Sumbawanga, Nkasi, Songea,
|
|
|
|
Mbeya, Njombe, Dabaga na sehemu
|
Uyole soya 1
|
Novemba/Desemba
|
|
zenye mvua nyingi/ndefu
|
|
|
|
|
|
|
2
|
Sumbawanga, Songea, Mbeya,
|
|
|
|
Njombe na sehemu zenye mvua
|
Bossier
|
Januari
|
|
nyingi/ndefu
|
|
|
3
|
Ileje, Mbarali, Chunya, Mtwara na
|
|
|
|
sehemu zenye mvua kidogo na fupi
|
Bossier
|
Novemba/Desemba
|
|
|
|
|
4
|
Morogoro na Tanga
|
Bossier
|
Februari na Machi
|
Nafasi
ya kupanda
|
Mmea wa soya baada ya kuota |
Mkulima
anashuriwa kupanda soya kwa nafasi zinazo pendekezwa na wataalamu. Nafasi hizo
ni sentimeta 10 kwa sentimita 45 kwa soya fupi kama
bossier na kwenye sehemu zenye rutuba hafi fu. Aidha, tumia sentimeta 10 kwa
sentimita 60 kwa soya ndefu kama Uyole Soya 1 na kwenye sehemu zenye rutuba
nyingi.
Panda mbegu moja kila shimo na zifukiwe kwa kina cha
sentimeta mbili hadi sentimita tano ili zisiharibiwe au kuliwa na wanyama kama
panya. Mkulima ahakikishe kuwa soya inapandwa kwenye udongo wenye unyevu wa
kutosha; haitakiwi kabisa kupanda soya kwenye udongo mkavu au kuloweka soya
kabla ya kupanda.
Palizi
Soya ni
zao ambalo huzongwa na magugu hususani ikiwa katika hatua za mwanzo za ukuaji.
Kwa hiyo mkulima anashauriwa kuwahi palizi katika kipindi cha wiki mbili baada
ya soya kuota. Palizi ya mara ya pili inategemeana na kiwango cha magugu
shambani. Endapo magugu yatakuwa yamefunikwa na majani ya soya palizi ya pili
inaweza isihitajike kwa kuwa soya iliyopandwa kwa
nafasi zinazotakiwa hukua na kufunika magugu yote na hivyo palizi ya
pili kutohitajika.
Soya ikipandwa kwa nafasi pana na
isiyotakiwa haikui kufi kia kiwango cha kufunika magugu na hivyo
kulazimisha palizi ya pili kufanyika. Magugu katika shamba la soya yanaweza
kudhibitiwa pia kwa katumia dawa ya kuzuia magugu kama GALEX; hata hivyo inafaa
kufuata maelekezo ya kutumia ya dawa husika.
|
Shamba la soya iliyopandwa kitaalam |
Soma Tajirika na SOYA sehemu ya pili
Labels: KILIMO BORA