....kutokana na mavuno ya soya, mkulima anaweza kupata mapato mengi ukilinganisha na mazao kama mahindi na maharage kwa eneo lililosawa na eneo la soya. Ukweli huu unabainishwa na tathmini iliyofanyika mwaka wa 2005 na Wizara ya Kilimo na Chakula, juu ya hali kilimo cha soya nchini.
4. WADUDU, MAGONJWA NA WANYAMA WAHARIBIFU
Wadudu
|
Wadudu mafuta (Aphids) |
Kwa
sasa, nchini Tanzania soya haishambuliwi sana na wadudu kama ilivyo sehemu
nyingine ambako zao hilo hulimwa kwa wingi. Hata hivyo endapo wadudu watatokea
mkulima anashauriwa kutumia dawa za wadudu kama Thiodan 35% EC na Sumithion 50%
EC kwenye kipimo cha mililita 40 za dawa na lita 20 za maji au kipimo kinacho
pendekezwa katika dawa husika. Upuliziaji wa dawa ufanywe kulingana na kiasi
cha mashambulizi ya wadudu kwenye mazao. Tofauti na mazao kama mahindi na
maharage, hakuna wadudu
waharibifu
wa soya ghalani. Hivyo zao hilo linaweza kutunzwa kwa muda mrefu ghalani bila
kuwa na athari za wadudu. Kwa mkulima na wafanyabiashara, kutokuwepo wadudu
waharibifu ghalani kunapunguza gharama za utunzaji hadi bei nzuri itakapofi
kiwa.
|
Mmea wa soya ulioshambuliwa na wadudu mafuta |
Magonjwa
|
Ugonjwa wa blait wa bakteria |
|
Kama
ilivyo kwa wadudu, magonjwa ya soya ni machache. Hata hivyo magonjwa ambayo
hutokea kwa nadra ni yale yanayotokana na vimelea vya ukungu (fungus) na bakteria.
Magonjwa hayo huenezwa kwa mbegu, masalia ya mimea shambani na wadudu mafuta (aphids).
Hivyo ni
bora kwa mkulima kuzingatia kanuni za kilimo bora au kupata ushauri wa
kitaalamu ili kuepukana na magonjwa hayo. Njia mojawapo ya kuzuia kuenea kwa
magonjwa katika zao la soya ni kupanda mbegu safi na zilizopendekezwa mahali
husika. Aidha, panda kwa mzunguko (crop rotation) kwa kutumia mazao
yasiyoshambuliwa na magonjwa ya soya kama alizeti na mahindi.
Wanyama
waharibifu
Kwa
kawaida soya hupendwa sana na panya wa shambani na ghalani. Wanyama wengine ni
pamoja na sungura, paa, swala, n.k. Mkulima anashauriwa kutumia mbinu na njia
mbalimbali zikiwemo za asili, kukabiliana na wanyama hao bila kuharibu
mazingira.
Uliikosa Part 1? Soma hapa
5. KUVUNA, KUPURA NA KUHIFADHI SOYA
Kuvuna
|
Soya tayari kwa kuvunwa |
Soya
huchukua wastani wa miezi mitatu hadi saba kukomaa kutegemea na aina, mahali
ilikopandwa na utunzaji wa shamba. Kwa mfano soya aina ya Bossier huchukua
miezi mitatu hadi minne kukomaa na aina ya Uyole Soya 1 miezi minne hadi
mitano. Dalili za soya kukomaa ni wakati majani yanapokuwa na rangi ya njano.
Anza kuvuna baada ya majani kuanza kupukutika.
Soya
ikikauka, maganda yake hupasuka na mbegu hupukutikia chini. Kwa hiyo mkulima
anashauriwa kuwahi kuvuna soya mara inapokomaa na kuanza kukauka. Ili kuzuia
upotevu wa zao shambani, inashauriwa kuvuna majira ya asubuhi au majira ambayo
sio ya jua kali endapo soya imekauka na kuanza kupasuka wakati wa kuvuna.
Kupura/kupiga
Soya
haitakiwi kupigwa kwa nguvu kwa sababu mbegu zake hupasuka kirahisi. Mara baada ya kupura, ondoa takataka na uchafu mwingine kwenye soya
kwa kupepeta na kupembua. Kausha soya kufi kia wastani wa
asilimia 10 ya kiasi cha maji (moisture content) kisha ihifadhi ghalani
kwa matumizi au kusubiri soko.
Kuhifadhi
Hifadhi
soya baada ya kuhakikisha kuwa imekauka vizuri. Ni muhimu kuhifadhi soya mahali
pakavu ili soya isipate uvundo na kuharibu soya ya mbegu na ya chakula. Soya
inaweza kuhifadhiwa kwenye vihenge au kwenye magunia kama mazao mengine,
tofauti ni kutohitajika dawa ya kuhifadhia.
6. MAVUNO
NA MAPATO YATOKANAYO NA ZAO LA SOYA
Mavuno
Soya ina
uwezo wa kutoa kilo 1,500 hadi 2,500 kwa hekta kutegemea na aina, hali ya hewa,
rutuba ya udongo, matumizi ya mbolea na utunzaji kuanzia wakati wa kuchagua
mbegu, kulima, kupanda na kuvuna. Kiasi hicho cha mavuno ni sawa na kilo 600
hadi 1,000 kwa ekari moja.
Mapato
Kutokana
na mavuno ya soya, mkulima anaweza kupata mapato mengi ukilinganisha na mazao
kama mahindi na maharage kwa eneo lililosawa na eneo la soya. Ukweli huu
unabainishwa na tathmini iliyofanyika mwaka wa 2005 na Wizara ya Kilimo na
Chakula, juu ya hali kilimo cha soya nchini. Tathmini hiyo ilionyesha
kuwa wastani wa gharama za kuzalisha kilo moja ya soya kwa mikoa ya Nyanda za
Juu za Kusini hususan Songea Vijijini ni shilingi 130, kwa
hiyo kama mkulima atauza soya kwa wastani wa shilingi mia mbili (200) kwa kilo
moja bila gharama ya kusafi risha mbali na kijijini kwake anaweza kupata faida
ya kati ya shilingi 105,000 hadi 175,000 kwa hekta moja au
kati ya shilingi 42,000 na 70,000 kwa ekari moja. Hata hivyo mapato yanaweza
kuongezeka endapo mkulima atatunza na kuuza soya wakati bei imepanda kwa kuwa
soya inaweza kutunzwa muda mrefu bila kuharibiwa na wadudu. Nidhahiri kuwa zao
la soya linaweza kumuongezea mkulima kipato na kumuondolea
umaskini.
Soma Tajirika na Zao La Soya - Part 1
MAREJEO
1. File
NAL/S./17/124. (2005). Soybean in Southern regions of Tanzania. Dr.
Mponda, O. K. K. ARI Naliendele. Personal communication
2. Laswai,
H. S., Kulwa, K. B. M., Ballegu, W. R. W., Silayo, V. C. K., Ishengoma, C. G.;
Makindara, J. A.; Mpagalile, J. J. and Rweyemamu, C. L. (2005). Soya kwa lishe
bora. Virutubisho na matayarisho yake kwa mapishi mbalimbali. SUA NORAD Focal
Programme.
3.
Mhagama, G. (2005). Soya: The golden seed in Tanzania. Sunnhemp seed
bank. Mruma Centre, Peramiho Songea. Personal communication.
4. Madata,
C. (Januari, 2005). Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. ilimo bora cha soya nyanda
za juu kusini na Vyakula vya soya na mapishi yake: Soya kwa afya yako. Toleo la
Tatu.
Labels: KILIMO BORA