Je unamfahamu mdudu huyu hatari kwa maharage?

Funza wa vitumba ni nondo, na ni mdudu mharibifu maarufu wa kunde na maharage mengine kote Afrika Mashariki na Magharibi. Viwavi hula vitumba na maua, na kuingia ndani ya mifuko ya maharage na kuacha tundu kwenye mfuko wa maharage na kula mbegu.

Habari na pole na kazi ndugu yangu. Karibu tena leo katika muendelezo wa makala yetu ya kilimo bora cha maharage, wiki iliyopita tuliangazia katika kilimo bora cha maharage kwa ujumla wake tangu kuandaa shamba, kuchagua mbegu, kupanda mpaka kuvuna maharage, na niliahidi wiki hii kuangazia wadudu waharibifu na magonjwa ya maharage lakini kutokana na umuhimu nimeona kwamba leo tumtazame mdudu muharibifu sana wa maharage ambaye kama hata dhibitiwa basi anaweza kusababisha hasara ya 80% ya maharage yako yote shambani. Mdudu huyu anaitwa funza wa vitumba, fuatana nami hadi mwisho …

Utangulizi
Funza wa vitumba ni nondo, na ni mdudu mharibifu maarufu wa kunde na maharage mengine kote Afrika Mashariki na Magharibi. Viwavi hula vitumba na maua, na kuingia ndani ya mifuko ya maharage na kuacha tundu kwenye mfuko wa maharage na kula mbegu. 

Je huyu mdudu yukoje?
Nondo aliyekomaa hutaga mayai moja moja au katika makundi madogo juu ya maua au vikonyo vya maua na pia kwenye vichomozo vya mimea michanga. Mayai yana umbo la mduara dufu, rangi nyeupe na manjano nyepesi; yai moja linaonekana kama tone dogo la maji. Larvae, au viwavi, vinaweza kukua na kufikia urefu wa milimita 17-20. 

Funza-wa-vitumba
Nondo aliyekomaa

Viwavi huwa rangi ya kijani chepesi na madoa ya kahawia-meusi na kichwa ni rangi ya kahawia iliyokolea. Viwavi wachanga hupatikana katika makundi wanapokuwa katika hatua hii, lakini baadaye kupatikana kila mmoja kivyake. Viwavi wachanga hushambulia maua na majani, lakini viwavi waliozeeka wana uwezo zaidi wa kutembea na mara nyingi wanapatikana wakila na kutoboa na kuingia ndani ya mfuko wa mbegu ambapo hula mbegu zinazokua. Vinapokomaa viwavi huanguka kutoka kwa mmea mpaka mchangani ambapo hubadilika na kuwa pupa wakiwa chini ya takataka. 

Kiwavi-wa-funza-wa-vitumba
Kiwavi wa nondo akiwa ndani ya jumba la maharage (podo)

Mbawa za nondo ni nyeusi-kahawia na zina alama nyeupe juu ya mbawa za mbele na upana wa mbawa wa milimita 20-25. Nondo huchangamka usiku. Wakati wa mchana hupatikana wakipumzika upande wa chini wa majani na mbawa zao zikiwa zimetandazwa.

Kuna hatua nne katika mzunguko wa maisha: mayai, viwavi, pupae na nondo aliyekomaa. Kukua kwa mayai huchukua wastani wa siku 3, hatua ya viwavi huchukua wastani wa siku 13-14, hatua ya pupae siku 6-7 na nondo waliokomaa wanaweza kuishi kwa wastani wa siku 6-10. 

Maharage yanashambuliwa yakiwa katika hatua gani?
Maharage hushambuliwa na funza wa vitumba kuanzia wakati wa kutoa vitumba mpaka wakati wa kuvuna. Angalia matundu ya mviringo kwenye maua na pia majani yaliyokunjwa ambayo yamekwama pamoja. Fungua maua na uangalie viwavi. Mifuko ya mbegu itakuwa na tundu la wazi ambalo kiwavi aliingilia. Angalia mipira ya manjanokahawia nje ya mifuko ya mbegu; hiki ndicho kinyesi kilichoachwa na viwavi walipoingia ndani ya mfuko wa mbegu.

Athari-za-funza-wa-vitumba-kwenye-mapodo-ya-kunde
Athari ya funza wa vitumba kwenye mapodo ya kunde

Njia Za Kudhibiti Funza Wa Vitumba

Kinga – mambo ya kufanya kabla dalili kuonekana

Mbinu za kitamaduni: 

Kudhibiti – mambo ya kufanya baada ya dalili kuonekana

Mbinu za kitamaduni: 
Maua-yaliyoathiriwa-na-funza-wa-vitumba
Maua yalivyoathiriwa na funza wa vitumba

Mbinu za kikemikali: 

Hu undo mwisho wa Makala yetu kwa leo, je ungependa jumatatu ijayo tukuletee Makala gani? Weka comment yako hapa chini na usisahau kushare Makala hii.

Labels: