UVUNAJI
Zao la ndizi huweza kuanza kuvunwa katika kipindi cha miezi 9 hadi miezi 15 tangu kupandwa kwa chipukizi. Muda wa kuvunwa hutegemea hali ya hewa. Katika sehemu za joto ndizi huvunwa mapema zaidi kuliko sehemu za baridi. Pia migomba iliyopandwa kwa kutumia machipukizi huzaa mapema kuliko iliyopandwa miche iliyozalishwa kwa
chupa (tissue culture).
MATUMIZI YA
RIBONI
Riboni za rangi moja
(au alama ya kamba) hufungwa kwenye migomba ya umri mmoja mara tu inapoanza
kuchanua, na riboni ya rangi nyingine hufungwa kwenye migomba itakayoanza
kuchanua wiki mbili hivi zinazofuata na kuendelea hivyo ili kurahisisha
kuitambulisha mikungu ambayo itavunwa kwa wakati mmoja. Pia matumizi ya riboni
hurahisiha utunzaji wa kumbukumbu ili kujua ni lini na ni mikungu mingai itavunwa.
WAKATI
UNAOFAA KUVUNA
Mkungu wa ndizi
huweza kuvunwa katika hatua tofauti kulingana na matumizi, aina na mahitaji ya
soko. Mkungu huachwa kwenye mgomba mpaka vidole (matunda ) vimejaa. Uzito wa
mkungu hongezeka haraka katika wiki mbili za mwisho, ambapo migongo ya ndizi
hutoweka. Ndizi zinaweza kuvunwa zikiwa zimekomaa na zimeiva kwa kiasi cha asilimia
75 kwa ajili ya kusafirishwa mbali, pia zinaweza kuvunwa zikiwa kukomaa na
zimeanza kuiva kwa ajili ya soko la karibu, au zikiwa zimekomaa na kuiva kabisa
kwa ajili ya soko na matumizi ya nyumbani. Njia bora ya kukata mkungu, ni ile
inayohakikisha kuwa mkungu wa ndizi hauanguki chini na kuvunja, kuchubua au
kuharibu ndizi, jambo ambalo litapunguza ubora. Ukichelewa kuvuna ndizi
zinaweza kuharibiwa na ndege, wanyama, wadudu au kuibiwa.
|
Mkungu uliotayari kuvunwa |
UBORA WA
NDIZI
Ndizi zenye sifa
nzuri sokoni ni zile ambazo zimekomaa kwa kiasi kinachotakiwa na zenye vidole
vyenye urefu mzuri na visivyo na michubuko. Pia ziwe hazijashambuliwa na
magonjwa wala wadudu waharibifu.
KIASI CHA
MAVUNO
Mavuno ya ndizi
hutegemea zaidi aina ya migomba, hali ya hewa, utunzaji wa mimea shambani.
Mavuno huweza kufikia hadi tani 60 au zaidi kwa hekta kwa mwaka. Hata hivyo
mavuno mazuri kwa mkulima wa kawaida yasipungue kati ya tani 20 hadi 30 kwa
hekta kwa mwaka.
|
Mikungu ya ndizi iliyovunwa |
MAGONJWA
Wadudu wanaosumbua
zaidi hili ni Minyoo fundo (Banana nematodes), na Vifukuzi (Banana weevils).
|
Banana weevil |
|
Banana nematode |
UDHIBITI WA
MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU
Magonjwa na wadudu
hawa huweza kuepukwa kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji wa zao hili. kama
usafi wa shamba na kuchagua chipukizi bora. Au kupanda miche iliyozalishwa kwa
chupa (Tissue culture banana seedlings) Hata hivyo mara mataizo haya yakitokea
muone mtaalam wa kilimo aliye karibu ili aweze kukupa ushauri.
|
Migomba iliyoathiriwa na mnyauko wa migomba |
Dalili nyigine za
ugonjwa wa mnyauko wa migomba unaosababishwa na bakteria.
|
Shina la mgomba likitoa ute mzito |
|
Ndizi zenye rangi ya kuoza |
Ugonjwa wa mnyauko wa migomba ni ugonjwa hatar sana, umeua migomba mingi sana mkoani kagera tangu ulipoingia kwa mara ya kwanza. Huu ugonjwa ndio uliwafanya ndugu zetu Wahaya waache kutegemea ndizi kama zao lao kuu, na hivyo kuanza kulima mazao mengine ya chakula. Endelea kuusoma hapa...
Labels: KILIMO BORA, Migomba