Asili ya migomba ni nchi za Malaysia na India ambazo ziko Kusini Mashariki mwa Asia. Migomba inayolimwa sasa imetokana na migomba ijulikanayo kama Musa balbisiana ambayo asili yake ni India, na Musa acuminata ambayo asili yake ni Malaysia.
UTANGULIZI
Hapa Tanzania kilimo
cha migomba kimekuwepo Kwa miaka mingi. Kilimo hiki ni
maarufu sana kwa sababu zao la ndizi limekuwa likitumika kama chakula kikuu
kwa baadhi ya mikoa kama vile Kagera, Kilimanjaro na Mbeya na hivyo
kulifanya muhimu, kufuatia mazao ya mahindi, mpunga, mtama,
muhogo,viazi na mazao ya jamii ya kunde kama vile maharage.
Zao la ndizi linaweza
kuwa moja kati ya mazao ya biashara iwapo litazalishwa kwa
kufuata kanuni bora za uzalishaji wa zao hilo, ikiwa ni pamoja na kupanda
aina bora ya migomba inayozaa ndizi zinazotambulika
katika masoko ya kimataifa.
ASILI YA
MIGOMBA
Asili ya migomba ni
nchi za Malaysia na India ambazo ziko Kusini Mashariki mwa Asia.
Migomba inayolimwa sasa imetokana na migomba ijulikanayo kama Musa balbisiana ambayo asili yake ni India, na Musa acuminata ambayo asili yake ni Malaysia. Kutoka Malaysia na
India migomba ilifika Afrika Mashariki katika karne ya tano.
AINA ZA
NDIZI
Kuna aina nyigi sana
za ndizi. Nchini Tanzania ndizi zinazozalishwa, zipo za aina nyingi ambazo
hutofautiana kwa majina kutokana na eneo au mkoa unaozalisha. Hata hivyo zinaweza kugawanywa katika makundi mawili.
- Aina ambayo huliwa
kwa kuzichoma, kukaanga au kupikwa zikichanganywa na
vyakula vingine kama vile nyama.
Aina za ndizi hizo ni pamoja na Mzuzu,
Mshare, Matoke, Bokoboko na Mkono wa Tembo.
- Aina nyingine ni zile
ambazo huliwa kama matunda, aina hizo ni kama vile Kisukari,
Kimalindi, Mzungu na Mtwike.
Kuna aina nyingine za
ndizi ambazo kwa sasa huzalishwa hapa nchini ambazo zina fahamika
kwa ubora wake katika masoko ya ndizi ya kimataifa. Aina hizi
ni pamoja na Williams, Grand Naine, Pazz, Jamaica, Gold Finger. Nyingine
ni Uganda green, Embwailuma Giant na Chinese Cavendish.
MAENEO
YANAYOLIMWA MIGOMBA NCHINI
Nchini Tanzania mikoa
inayoshughulika na kilimo cha migomba na kuzalisha zao la
ndizi kwa wingi ni pamoja na Kagera, Kilimanjaro, Mbeya, Arusha,
Manyara, Mara, Tanga, Morogoro, Kigoma, na Pwani.
Hata hivyo zao hili
linaendelea kuenea katika mkoa mingine nchini ikiwa ni pamoja na Dar es
salaam, Mwanza, Ruvuma, Shinyanga na Lindi. Pia Dodoma na Singida. Kilimo cha migomba
kinaweza kufanyika katika kipindi chote cha mwaka kulingana na
kiasi na mtawanyiko wa mvua hasa mabondeni au kwa umwagiliaji.
MATUMIZI YA NDIZI
Kilimo cha migomba
kina faida nyingi, baadhi ya faida za migomba na zao la ndizi ni: -
- Zao la chakula
- Zao la Biashara
- Kutengenezea pombe
- Kulisha mifugo
- Kutengenezea mbolea
(mboji)
- Matandazwa shambani
(mulch)
- Kutoa kivuli
- Kutoa nyuzi
- Kutengenezea vitu vya
sanaa
- Kamba
- Kufungia vitu
- Malighafi ya
kutengeneza vyakula na vinywaji mbalimbali.
- Dawa
- Majani kama miamvuli,
sahani, vikombe na kata
- Kuezekea.
Ndizi kwa ajili ya
chakula hutumika kwa kutengeneza vitu mbalimbali
- Makangale (Banana
figs)
- Poda (Powder)
- Chenge (chips)
- Jeya (flakes),
- Juisi,
- Lahamu (jam)
- Vinywaji baridi, kama
soda
- Mvinyo (Wine)
- Pombe kali
- Hamira
Soma kilimo cha migomba part 2 hapa
Je, wewe unalima migomba au unapenda kulima siku moja? Ulishawahi kukutana na changamoto yoyote katika kilimo cha migomba? Acha comment yako hapa chini.
Labels: KILIMO BORA, Migomba