Vitunguu vinashambuliwa na magonjwa na wadudu mbalimbali na kusababisha upungufu na ubora wa mazao. Ili kudhibiti tatizo kwanza shamba likaguliwe mara kwa mara kuona dalili za mashambulizi.
MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU WA VITUNGUU
Vitunguu
vinashambuliwa na magonjwa na wadudu mbalimbali na kusababisha upungufu na
ubora wa mazao. Ili kudhibiti tatizo kwanza shamba likaguliwe mara kwa mara
kuona dalili za mashambulizi. Endapo kuna dalili za mashambulizi, chukua hatua
za kuzuia kabla uharibifu mkubwa haujatokea.
MAGONJWA YA VITUNGUU
a) Baka zambarau
(Puple Blotch)
Ungonjwa huu
unasababishwa na kuvu (fangasi). Chanzo kikubwa cha ugonjwa ni mbegu zenye
ugonjwa. Pia ugonjwa unajitokeza wakati kuna ukungu na unyevunyegu mwingi
hewani has wakati wa masika. Kiasi cha 60-80 % ya mazao yanaweza kupotea kama
ugonjwa hautadhibitiwa.
Dalili za
ugonjwa ni:-
· Kujitokeza
madoa meupe yaliyodidimia kwenye majani na kwenye mashina ya mbegu
· Rangi ya
zambarau kuwepo katikati ya doa jeupe.
· Majani
kuanguka
· Mashina ya
mbegu kuanguka kabla ya mbegu kutengenezwa
|
Baka Zambarau kwenye majani ya vitunguu
|
Njia za
kudhibiti:-
· Kupanda mbegu
safi
· Kupanda
vitunguu kwa kutumia mzunguko wa mazao
· Kuteketeza
msalii ya vitunguu baada ya kuvuna
· Kupulizia dawa
zilizopendekezwa kama Dithane M45 na Ridomil MZ. Dawa hizi zinachanganywa na
povu la sabuni ili zijishike kwenye majani.
b) Ubwiri
vinyoya (Downy Mildew)
Ugonjwa huu
unasababishwa na kuvu (fangasi) na kuenezwa na mbegu, hewa na masalia ya
vitunguu.
Unajitokeza
wakati kuna unyevunyevu mwingi hewani hasa wakati wa masika na dalili zake ni
kama zifuatazo:-
· Madoa yenye
umbo la yai, rangi ya njano iliyofifia hujitokeza kwenye majani makukuu na
kusambaa mpaka kwenye majani machanga.
· Baada ya siku
chache madoa ya njano yanafunikwa na ukungu wa rangi ya kijivu.
· Majani
yanasinyaa na kufa kuanzia kwenye ncha.
· Shina la mbegu
huzungukwa na vidonda na kusababisha kichwa cha mbegu kuanguka.
|
Ugonjwa wa ubwiri vinyoya kwenye vitunguu
|
Njia za
kudhibiti ugonjwa ni kama zifuatavyo:-
· Kupanda mbegu
safi
· Kupanda
vitunguu kufuata mzunguko wa mazao
· Kupulizia dawa
za ukungu kama dithane m45 na ridomil mz.
· Kuweka shamba
safi
· Kuteketeza
mabaki ya vitunguu
· Kumwagiliaji
maji nyakati za asubuhi au jioni
c) Kinyausi
(Damping – off)
Ugonjwa huu
unasababishwa na fangasi na kuenezwa na udongo, mbegu na masalia ya mazao.
Ugonjwa huu unasababisha mbegu kuoza kabla ya kuota na kunjauka kwa miche baada
ya kuota. Ugonjwa unajitokeza hasa kitaluni ikiwa hali ya hewa ina unyevunyevu
na udongo una maji maji.
Njia za kudhibiti
ni kama zifuatazo:-
· Mbegu ziwe
safi na ziwekwe dawa ya thiram
· Kutumia
mzunguko wa mazao
· Kusia mbegu
kwa nafasi za kutosha
· Kuepukana na
kubananisha miche kitaluni
· Kuepukanana na
kumwagilia maji wakati wa jua kali au wakati kuna ukungu
d) Virusi njano
vya vitunguu (Onion yellow Dwarf virus)
Ugonjwa huu
unasababishwa na virusi na kuenezwa na wadudu aina ya vidukari (wadudu mafuta).
Dalili za
ugonjwa ni:-
· Mistari ya
rangi ya manjano kwenye majani.
· Kujikunja kwa
majani
· Majani kugeuka
rangi ya manjano na kuanguka
· Mimea mzima
kudumaa, kujikunja na kufa.
|
Virusi njano kwenye vitunguu
|
Njia za
kudhibiti ugonjwa huu ni:-
· Kutumia mbegu
safi
· Kuweka shamba
katika hali ya usafi
· Kuzuia wadudu
kwa kupulizia dawa kama selecron, actellic, dursban nk.
WADUDU WAHARIBIFU WA VITUNGUU
Wadudu
wanaosababisha uharibifu mkubwa kwenye vitunguu ni chawa wekundu (thrips) na
sota (cutworms). Wadudu wengine ni pamoja na utitiri wekundu (red spider mites)
na vipekecha majani (leaf miner)
a) Wadudu chawa
(thrips)
Uharibifu
uletwao na wadudu chawa, unatofautiana msimu mmoja na mwingine kutegemeana na
hali ya hewa. Mvua kidogo pamoja na joto kali unasababisha mlipuko wa wadudu.
Wanshambulia majani kwa kukwaruakwarua na kunyonya maji hivyo kusababisha
majani kuwa na rangi ya fedha/siliver na baadaye majani yanakauka. Upungufu
mkubwa wa mazao unatokea.
|
Wadudu chawa (thrips) kwenye majani ya vitunguu
|
Njia ya
kudhibiti hawa wadudu ni:-
· Kuweka shamba
katika hali ya usafi
· Kuondoa magugu
shambani na yanayozunguka shamba la vitunguu
· Kupulizia dawa
ya wadudu kama karate, selecron, dursban, actellic.
b) Sota
(Cutworms)
Sota au viwavi
wa nondo wanasababisha uharibifu mkubwa. Viwavi wanakata mashina ya miche
michanga sehemu ya chini ya shina juu ya ardhi. Sota wanapendelea kula wakati
wa usiku na mchana kujificha kwenye ardhi karibu sana na sehemu waliokata
shina. Uharibifu huu unapunguza sana idadi ya mimea shambani na kuleta upungufu
wa mazao. Wadudu hawa wanadhibitiwa kwa kupulizia dawa kama; Karate Dursban na
Actellic na kuweka shamba katika hali ya usafi.
|
Sota kwenye jani la kitunguu
|
c) Utitiri
wekundu (Red spider mites)
Hawa ni wadudu
wadogo sana, ambao wanajificha upande wa chini wa majani. Wanafyonza maji maji
kwenye majani na kusababisha majani kuwa na rangi nyeupe. Wadudu hawa
wanatengeneza utando mweupe kuzunguka majani na mashina. Mmea unashindwa
kutengeneza chakula na baadaye inakufa.
|
Utitiri mwekundu
|
Njia ya
kudhibiti:
· Kupulizia dawa
za wadudu Karate na Selecron.
· Kuteketeza
masalia ya mazao
· Kutumia
mzunguko wa mazao
d) Vipekecha
majani (leaf miner)
Hawa ni aina ya
inzi wadogo, ambao viwavi wake wanashambulia majani, kwa kupekecha na
kutengeneza mitandao wa mitaro kwenye majani. Viwavi wanashambulia majani na
kusababisha majani kukauka. Upungufu mkubwa wa mazao hutokea.
|
Athari ya vipekecha majani |
Njia ya dhibiti:
· Kupulizia dawa
ya wadudu kama karate Selecron na Dursban
· Kuteketeza
masalia ya mazao
· Kutumia
mzunguko wa mazao
Kwa upande wako ni unasemaje juu ya changamoto hii ya magonjwa na wadudu katika klimo cha zao hili la vitunguu? Usisahau kuacha comment yako hapa chini.
Labels: VITUNGUU, WADUDU NA MAGONJWA YA MIMEA