>>Uchaguzi wa Kuku bora
Ili upate kundi lenye
kuku bora huna budi uchague jogoo bora na matetea bora wa kuzalisha kundi lako.
Angalia sifa zifuatazo unapochagua:
i. Tetea na jogoo wawe na umbo kubwa.
ii. Wanaokua haraka.
iii. Wenye uwezo wa kustahimili magonjwa.
iv. Matetea wanaoweza kutaga mayai mengi
v. Matetea wanaweza kuatamia na hatimaye
kutotoa vifarangakwa wingi na kuvilea
vi. Jogoo unaowachagua kwa ajili ya matetea
au makoo yako wasiwe na uhusiano wa damu.
Ukiishachagua wazazi wa
kundi lako changanya jogoo na matetea kwa uwiano wa jogoo mmoja kwa matetea 10
hadi 12. Ukiwa na matetea 20 utahitaji kuwa na jogoo wawili.
Nchini kwetu zipo aina tofauti za kuku
wa asili ambao wana sifa tofauti. Wafugaji wengi hufuga kutegemeana na uwezo wa
kuku kuhimili magonjwa ,kuwa na uzito mkubwa, utagaji wa mayai mengi n.k. Koo
za kuku wa asili wenye sifa za namna hii ni aina ya Bukini , Kuchi, Kuchere na
wa Kawaida wasio na ukoo maalum. Hawa kwa ujumla wao wakitunzwa vizuri wana
uwezo wa kufanya vyema katika mazingira ya ya nchi hii kwa sababu
wameishayazoea.
>>Kuatamia na kuangua mayai:
Baada ya jogoo kupanda
matetea au makoo, hawa watataga mayai. Mayai yanaweza kutotoleshwa kwa njia ya
asili au kwa kutumia vifaa vya kutotolesha.
>>Kutotoa
kwa njia ya asili
Hii inafanyika kwa kuku kuatamia mayai kwa hatua
zifuatazo.
>>>Kuandaa kiota
•
Kiota kiandaliwe kabla kuku hajaanza
kutaga kwa kukiwekea nyasi kavu na kuzisambaza kwa kutengeneza muundo wa kata
au sahani iliyozama kidogo.
|
Kiota cha kuku |
• Kiota kinyunyiziwe dawa ya unga kuua
wadudu kabla na baada ya kuweka nyasi. Iwapo kuku atajiandalia kiota chake
mahali panapofaa aachwe hapo ila kiota kiwekewe dawa ya kudhibiti wadudu.
Maandalizi ya kuku anayetaka kuatamia
Dalili za kuku
anayetaka kuatamia ni:
o Anatoa sauti ya
kuatamia.
o Ushungi
wake umesinyaa.
o Hapendi kuondoka kwenye kiota.
o Hupenda kujikusanyia mayai mengi
Kuku wenye dalili za kutaka kuanza kuatamia
akaguliwe ili kuhakikisha kuwa hawana wadudu kama utitiri, chawa, viroboto n.k.
wanaoweza kumsumbua wakati wa kuatamia. Akiwa na wadudu watamsumbua hataweza
kutulia kwenye kiota na kuatamia vizuri. Matokeo yake ataangua vifaranga
wachache. Hivyo walio na wadudu wanyunyizie dawa ya unga kabla hawajaanza
kuatamia ili kudhibiti tatizo hili.
>>Kuatamia
Kuku anapotaga mayai
yaondolewe na kubakiza moja kwenye kiota ili kumwita kuku kuendelea kutaga.
Kuku akiwa tayari kuatamia awekewe mayai kwa kuatamia. Kwa kawaida kuku mmoja
anaweza kuatamia vizuri mayai 10 hadi 13 kwa wakati mmoja.
Kipindi cha kuangua
mayai ni kuanzia siku 20 baada ya kuatamia. Ukitaka kutotolesha vifaranga wengi
kwa wakati mmoja, kuku akianza kutaga yakusaye mayai yake na kumbakizia yai
moja ili aendelee kutaga.Mayai utakayokusanya yaweke mahali pasipo na mwanga
mwingi na penye ubaridi kiasi.
Fanya hivi kwa kuku
kadhaa wanaotaga ndani ya muda unaokaribiana. Kila atakayeonyesha dalili ya
kuanza kuatamia muwekee mayai kati ya 10 na 12 aatamie. Kwa njia hii wataatamia
na kuangua ndani ya kipindi kimoja. Na utapata vifaranga wengi wa umri mmoja
hatimaye kuuza kuku wengi kwa pamoja.
>>Kulea Vifaranga
Baada ya vifaranga
kutotolewa waache na mama yao mahali penye usalama kwa muda wa mwezi moja mbali
na mwewe, vicheche, paka, kenge, n.k. Hakikisha wanapata maji na chakula cha
kutosha muda wote.
>>>Kulea
vifaranga kwa kumtumia kuku
Njia nyingine ni
kuwaweka vifaranga mahali pazuri na kuwafunika na tenga ili kuzuia mwewe wakati
wa mchana kwa kuhakikisha kuwa hawapigwi na jua wala kunyeshewa mvua.Wakati wa
usiku warejeshe kwa mama yao ili awakinge na baridi. Fanya hivi hadi wafikie
umri wa mwezi mmoja ndipo uwatenge na mama yao.
>>>Pia
unaweza kutumia kifaa maalum cha kulelea vifaranga (kitalu/brooder)
mara baada ya kuanguliwa. Katika kitalu wanapatiwa joto wanalohitaji. Kifaa
hiki kinaweza kutengenezwakwa karatasi ngumu itumikayo kutengeza dari.
Au
Katika mazingira ya
kijijini unaweza kutengeneza wigo wa mduara kwa magunia. Upana wake uwiane na
wingi wa vifaranga ulionao na kina chake kama mita moja. Ukuta wake uwe na
tabaka mbili za magunia hayo zilizoachana kwa nafasi ya inchi tatu au nne. Kati
kati ya nafasi hiyo jaza maranda ya mbao au pumba za mpunga. Tayari utakuwa umepata
kitalu cha kulelea vifaranga.
Ndani ya kitalu weka taa ya chemli ya kutoa joto
linalohitajika kwa vifaranga. Fuatilia tabia ya vifaranga wanapokuwa katika
kitalu.
Wakiisogelea sana taa
ina maana joto halitoshi, ongezea joto kwa kupandisha utambi. Wakienda mbali
sana na taa, joto limezidi punguza. Kitalu kikiwa na joto zuri vifaranga
watatawanyika kote katika kitalu na kuonyesha kuchangamka.
Mama yao akitengwa na
vifaranga arudishwe kwenye kundi lenye jogoo, atapandwa na kurudia kutaga
mapema. Kwa njia hii kundi la kuku litakuwa kubwa kwa muda mfupi. Kwa kawaida
vifaranga wengi hufa kabla ya kufikisha miezi miwili kutokana na baridi, kuliwa
na wanyama wengine na magonjwa.
Ili kudhibiti magonjwa, vifaranga wapewe chanjo
dhidi ya magonjwa yafuatayo:
a. Kideri
( New castle) siku ya 3 baada ya kuanguliwa, rudia
baada ya wiki tatu kisha uchanje kila baada ya miezi mitatu.
b. Kuhara
damu au rangi ya ugoro (Coccidiosis) : Wapewe kinga kwa dawa
ya Amprolium kwa siku 3 mfululizo wanapofikisha umri wasiku 7 baada ya
kuanguliwa.
c. Gumboro
wanashusha
mbawa na kujikusanya pamoja kwa baridi, pia wanaharisha nyeupe.Hutokea
kuanzia wiki ya 2 hadi ya 18.Wapewe chanjo siku ya 10 hadi ya 14 baada ya
kuanguliwa na rudia baada ya siku 28 na 42. Kwa magonjwa mengine angalia
maelekezo sehemu ya magonjwa ndani ya mwongozo huu.
Vifaranga wapewe
chakula kilichoelezwa katika sehemu ya tatu ya kijitabu hiki na maji safi ya
kutosha wakati wote kwa muda wa miezi miwili. Baada ya hapo wanapewa chakula
cha kuku wanaokua.
Kuku wakikaribia
kupevuka wakiwa na miezi mitatu hadi minne tenganisha temba na majogoo ili
kudhibiti kuku wenye uhusiano wa damu wasipandane wao kwa wao. Wakipandana na
mayai yao yakianguliwa hawatatoka vifaranga wenye sifa nzuri mfano: ukuaji wao
utakuwa hafifu kuliko wazazi wao, uwezo mdogo kuhimili magonjwa na wengine
wanaweza kuwa na ulemavu. Pia zingatia matemba hao wasipandwe na baba yao.
Vilevile majogoo hao wasimpande mama yao.
>>Ulishaji
Kuku kama mifugo
mingine uhitaji chakula chenye virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini ili
kukua upesi na kuwa na na afya nzuri . Chakula kinachofaa ni mchanganyiko wa
viini lishe mbalimbali vyenye kazi tofauti mwilini. Kila kiini lishe hakina
budi kiwe katika kiwango sahihi kulingana mahitaji ya mwili wa kuku katika umri
tofauti.
Kuku
anahitaji chakula chenye viini lishe vifuatavyo:
Kiini Lishe
|
Kinapatikana Katika
Chakula Gani
|
Kazi Yake Mwilini
|
|
Wanga
|
Pumba,Chenga
|
za nafaka
|
kama
|
Kutia nguvu mwilini
|
|
mahindi,
mtama.
|
|
|
|
|
|
|
|
Mafuta
|
Mashudu
yanayopatikana baada ya
|
Kutia
|
nguvu
|
na
|
joto
|
|
kukamua mbegu
za mafuta kama
|
mwilini
|
|
|
|
|
alizeti,
karanga n.k
|
|
|
|
|
|
|
Protini
|
Mashudu ya
karanga au alizeti.Damu
|
Kujenga
|
mwili
|
na
|
|
iliyokaushwa ya
|
wanyama
|
kama
|
kukarabati mwili
|
|
|
mbuzi, ng’ombe
n.k. Mbegu za jamii
|
|
|
|
|
|
|
ya mikunde
kama maharage, kunde,
|
|
|
|
|
|
|
soya....
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Vitamini
|
Majani mabichi
kama mabaki ya
|
Kulinda
|
mwili.
|
Majani
|
|
mboga za
majani, michicha ya porini,
|
mabichi
|
pia
|
huwezesha
|
|
majani mabichi
ya mipapai, majani ya
|
kuku kutaga mayai yenye
|
|
Lusina n.k.
|
|
|
kiina
|
cha njano,
|
rangi
|
|
|
|
|
ambayo huwavutia walaji
|
|
|
|
|
wengi.
|
|
|
|
|
Madini (calsium
|
Unga wa dagaa,
|
unga wa
|
mifupa
|
Kujenga
|
|
mifupa,
|
na Fosforas)
|
iliyochomwa,
chokaa
|
|
kutengeneza
|
maganda
|
|
|
|
|
ya mayai
|
|
|
|
Mfano
wa kuandaa vyakula vya makundi tofauti ya kuku
Kwa
Vifaranga
Kwa vifaranga vya tangu kutotolewa hadi miezi miwili
tengeneza mchanganyiko ufuatao. Huu ni mfano mmojawapo wa kuandaa kilo 100 za
chakula cha vifaranga. Iwapo utahitaji kuandaa jumla ya kilo 50 za chakula
tumia nusu ya vipimo vilivyoainishwa katika jedwali hili.
Wastani wa mahitaji ya kuku wakubwa 50 kwa siku ni
kilo 5. Chakula hiki ukigawe katika sehemu mbili na kuwapatia nusu asubuhi na
nusu ya pili mchana.
Vifaa
|
Kiasi kwa kilo
|
|
Dagaa (unga au
vichwa vya dagaa)
|
12 hadi 15
|
|
Chenga za
nafaka kama mahindi au mtama n.k
|
40
|
|
Mashudu
|
20
|
|
Pumba
|
24
|
|
Chokaa
|
2
|
|
Unga wa
Mifupa,Madini ( Premix)
|
2
|
|
Chumvi
|
Robo kilo
|
|
Mchanga
|
1
|
|
Jumla
|
Kilo 100
|
|
|
|
|
Kwa
kuku wanaokua (baada ya miezi miwili ).
|
|
|
|
|
|
Vifaa
|
Kiasi kwa kilo
|
|
Dagaa (unga au
vichwa vya dagaa)
|
7
|
|
Chenga za
nafaka kama mahindi au mtama n.k
|
30
|
|
Mashudu
|
20
|
|
Pumba
|
39
|
|
Chokaa
|
2
|
|
Unga wa Mifupa,Madini
( Premix)
|
2
|
|
Chumvi
|
Robo kilo
|
|
Mchanga
|
1
|
|
Jumla
|
Kilo 100
|
|
|
|
|
Kama umeamua kufuga
kuku kwa mtindo wa kuwaacha huru wajitafutie chakula (huria) unaweza kuwapatia
vifaranga nyongeza ya protini.Utafanya hivyo kwa kuwachanganyia vumbi au vichwa
vya dagaa kiasi cha kikombe kimoja vilivyotwangwa pamoja na pumba ya mahindi
vikombe vitano.
>>Maji
ya Kunywa
Mfugaji ahakikishe
anawapatia kuku maji masafi ya kunywa na ya kutosha kila siku. Vyombo vya maji
ya kunywa budi visafishwe vizuri kila siku. Hii itasaidia sana kudhibiti
magonjwa yanayoweza kutokana na vimelea vya magonjwa vinavyostawi katika maji
yasiyo safi. Kuku wanaweza kuwekewa maji katika aina tofauti ya vyombo
kutegemea na urahisi wa kupatikana mfano sufuria, ndoo za plastik zilizokatwa
kuruhusu kuku kunywa bila kuchafua.
>>Usafi
katika banda
Matandazo yanayowekwa
katika sakafu ya banda la kuku hayana budi yageuzwe mara kwa mara kwa wastani
wa kila baada ya miezi miwili au mitatu . Wakati mwingine ni kabla ya kipindi
hiki muda wowote yanapoloana na maji. Matandazo uharakisha kukauka kwa unyevu
katika banda unaotokana na kinyesi cha kuku na pia zaidi na maji yanayomwagika.
Usafi
katika banda utasaidia kudhibiti kwa kiasi kikubwa magonjwa mbalimbali.
>>Kuokota mayai
Usiyaache mayai ndani
ya viota kwa muda mrefu, yaokote mara kwa mara ili kuepuka kuharibiwa kwa mayai
hayo na kuku wenyewe. Kuku wanayo tabia ya kula mayai yao ikiwa chakula
unachowapa kina upungufu wa protini.
Vilevile kiasi cha
mwanga unaoingia ndani ya banda kikizidi kuku hula mayai au kudonoana wenyewe
kwa wenyewe.Uonapo dalili za namna hii kwenye kundi lako punguza kiasi cha
mwanga kwa kuziba sehemu za madirisha kwa vipande vya magunia au vipande vya
makasha ya karatasi ngumu.
Kama ilivyoelezwa awali
kuku wapewe majani mabichi ya kutosha mara kwa mara ili wawe wanakula hayo
badala ya kudonoana.
Pia fuatilia
kuhakikiksha kama chakula kina protini ya kutosha. Kama tatizo la kudonoana na
kula mayai litaendelea omba msaada kwa mtaalam wa mifugo akuelekeze jinsi ya
kuwakata au kuwachoma midomo.
Labels: UFUGAJI, UFUGAJI WA KUKU