1. Kideri (NewCastle)
|
Virusi
|
- Kukohoa, kupumua kwa shida
- Mwili kukosa nguvu
- Shingo kujikunja
- Kuharisha kijani
- Kuku wengi hufa
- Kuhara damu
|
- Vifaranga wachanjwe katika juma lao la kwanza
- Wachanjwe tena wanapofikisha umri wa miezi minne na nusu
- Kuku wachanjwe kila baada ya miezi mitatu
|
2. Kuhara damu (Coccidiosis)
|
Bakteria
|
- Kuku hujikusanya, hawachangamki, hushusha mbawa
|
- Tunza usafi katika banda
- Lisha vifaranga chakula kilichochanganywa na dawa ya kinga ya Coccidiosis kama vile Amprolium au Salfa
- Watenge kuku wote walioambukizwa na uwape dawa kama Amprolium au salfa au Esb3
|
3. Ndui ya kuku (Fowl Pox)
|
Virusi
|
- Malengelenge kwenye kishungi, kope za macho na sehemu zisizokuwa na manyoya
|
- Kuchannja kuku wote wakiwa na umri wa miezi miwili
- Watenge kuku wote walio ambukizwa na uwape ANTIBIOTIC kama OTC Plus au salfa
|
4. Mafua ya kuku (Fowl Cryza)
|
Bakteria
|
- Kuku huvimba uso
- Kamasi hutiririka puani na mdomoni
- Kuhema kwa shida sana hata kukoroma
|
- Usafi wa banda
- Kuchanja kuku wote kabla hawajaambukizwa
- Na kama ni tatizo sugu basi watibu wote waliougua kwa kuwapa ANTIBIOTICS kama Sulphamethazine, Steptomycin na Vitamin
|
5. Kuharisha Nyeupe
|
Bakteria
|
- Kuharisha nyeupe na
- Kupungua hamu ya kula
|
- Usafi wa vyombo na banda kwa ujumla
- Watenge kukuu wagonjwa
- Tumia dawa kama Furazolidone au Sulfadimidine
- Hata vitunguu swaumu menya robo kilo utwange na uchanganye na maji lita moja. Chuja halafu uwape haya maji kwa muda wa wiki moja
|