"....Ili ufanikiwe katika ufugaji wa kuku, ni muhimu sana kulifahamu vyemi kundi la kuku wako. Ukilifahamu vema kundi lako utaweza kuchagua kuku bora wa kuzalishia kwa kuangalia ubora wa wazazi wao."
KUSIMAMIA UFUGAJI WAKO
>>Kutunza kumbukumbu
Ili ufanikiwe katika
ufugaji wa kuku, ni muhimu sana kulifahamu vyemi kundi la kuku wako.
Ukilifahamu vema kundi lako utaweza kuchagua kuku bora wa
kuzalishia kwa kuangalia ubora wa wazazi wao. Kufahamu historia ya afya ya
kundi, kwa mfano:
• Umri ambapo vifaranga vilipata chanjo.
• Ni chanjo ya aina gani.
• Magonjwa ambayo yamewahi kushuambulia
kundi, na dawa ulizotumia katika matibabu.
• ldadi ya kuku wanaokufa.
• Kukadiria kiasi cha chakula ambacho kuku
wako watahitaji kwa muda fulani na aina ya chakula.
• Kujua kila siku kuku wametaga mayai
mangapi.
• Kujua utahitaji muda gani kutunza kuku
toka vifaranga mpaka wanapofikia kuuzwa.
Ili uweze kufahamu mambo haya yote unahitaji
kutunza kumbukumbu.
Ufuatao hapa chini ni
mfano rahisi wa kutunza kumbukumbu za kuku tangu wangali vifaranga mpaka
wanapofikia uzito wa kuuzwa.
Mfano wa Kumbukumbu za ufugaji wa Kuku
i. Kumbukumbu
ya Vyakula
Tarehe
|
Kiasi cha
|
Chakula
|
Kundi / Umri wa
|
Maoni
(Gharama,
|
|
(Kilo)
|
|
kuku
na idadi yao
|
Kimetumika
kwa muda gani
|
|
|
|
|
nk)
|
|
15
|
|
Vifaranga
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
25
|
|
Wanaokua
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Jumla
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Hapa utaweza kujua
wastani wa matumizi ya chakula kwa idadi ya kuku na kwa kipindi husika.
Tarehe ya kuuza……………………….
Idadi iliyouzwa……………………………
Umri wa kuku wakati wa
kuwauza................
Mapato kutokana na kuuza……………………
ii. Kumbukumbu
ya Kutibu Magonjwa
Tarehe
|
Magonjwa
|
Tiba
|
Maoni
(vifo, gharama nk)
|
|
|
|
|
3.7.2009
|
coccidiosis
|
teramycin
|
|
5.9.2009
|
mdondo
|
furazolidone
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Kumbukumbu hii
itakusaidia kujua magonjwa yanayosumbua mara kwa mara na kwa kipindi kipi. Pia
na dawa inayosaidia zaidi kwa tatizo husika.
iii. Chanjo
au Kudhibiti magonjwa
Tarehe
|
Ugonjwa/Wadudu
|
Dawa
|
Gharama
|
|
|
|
|
6.8.2009
|
Viroboto
|
Kunyunyiza
doom powder au sevin powder
|
|
5.10.2009
|
coccidiosis
|
Amprol
katika maji, kinga dhidi ya
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
>>Jinsi ya Kufahamu Faida Unayopata
IIi uweze kufahamu
faida unayopata kutokana na ufugaji wa kuku inakupasa kutunza kumbukumbu za
matumizi na mapato ya kila siku.
Upande wa matumizi ingiza
• Gharama ya kununua vifaranga (kama
walitotolewa hapo hapo nyumbani inafaa ukadirie gharama hiyo).
• Kama unatengeneza na kuchanganya wewe mwenyewe
kadiria kwa kutumia bei za viungo ghafi.
• Gharama ya mafuta ya taa (kama uliwakuza
vifaranga kwa joto Ia taa).
• Gharama ya kusafisha banda kubadili
matandazo.
• Gharama za madawa ya kinga (chanjo) na
tiba.
Upande wa mapato ingiza mapato kutokana na:
•Gharama ya mayai yaliyotumiwa nyumbani.
•Mauzo ya mbolea kutoka katika banda.
Ufuatao ni mfano unaoonyesha jinsi ya
kuingiza taarifa hizi katika daftari la kumbukumbu ya Kutibu Magonjwa
Tarehe
|
Matumizi
|
Sh.
|
Tarehe
|
Mapato
|
Sh.
|
|
|
|
|
|
|
|
Kununua
vifaranga
|
6,000/=
|
|
Mauzo
ya mayai 10
|
1,500/=
|
|
30
@ 200/=
|
|
|
@150/=
|
|
|
Kununua
vyakula
|
1,500/=
|
|
Mayai
na kuku
|
7,000/=
|
|
kilo
10 @150/=
|
|
|
waliotumiwa
|
|
|
|
|
|
nyumbani
|
|
|
Dawa
ya kukohoa
|
1,500/=
|
|
Mauzo
ya kuku 20
|
80,000/
|
|
1500/=
|
|
|
@
4000/=
|
|
|
Dawa
ya wadudu
|
1000/=
|
|
Mbolea
iliyouzwa
|
|
|
1000/=
|
|
|
|
|
|
……nk.
|
…..
nk
|
|
….
nk
|
|
|
|
|
|
|
|
Jumla
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Baada ya kufanya mauzo
yote ya kundi jumlisha matumizi yote na jumlisha na mapato yote katika kipindi
kizima cha kufuga.
Ili kufahamu faida uliyopata fanya
hesabu hii:
Jumla ya Mapato yote - Jumla ya Matumizi
yote = Faida
Katika biashara ya aina
yoyote mzalishaji hana budi afahamu mambo kadhaa ya msingi yatakayomsaidia
kufanya maamuzi ya kumuwezesha kupata faida ya juu katika biashara anayoifanya:
Kwanza kabisa ajiulize kama bidhaa
anayozalisha ina soko? Na kama soko lipo:
•Lipo wapi na hali ya miundombinu za
kulifikia iko vipi ( ili afahamu gharama ya kufika sokoni kama utaamua kuuzia
sokoni).
•Bidhaa inahitajika kwa wingi kiasi gani
na wakati gani sokoni
•Soko linahitaji bidhaa yenye sifa zipi (
ubora n.k. ili uzalishe sawa na matakwa ya soko n.k)
•Kama wanunuzi watakuwa na utayari
kununulia unakozalishia, je unao uwezo wa kutosheleza mahitaji yao (ili uweze
kujipanga kukidhi mahitaji kwa kuongeza uzalishaji au kwa kuungana na
wazalishaji wengine).
•Linganisha bei ya bidhaa sokoni na bei
ya kuuzia unakozalishia (ili ujue palipo na faida zaidi kwako baada ya kuondoa
gharama za kufuata soko) Ila ukiamua kuuzia sokoni hakikisha unao uwezo wa
kushindana na wauzaji wengine huko sokoni.
Majibu ya maswali haya
ndiyo yatakayokupa msingi wa kujipanga kiuzalishaji ili hatimaye upate faida.
Hivyo hata kabla hujaanza kuzalisha fahamu haya yaliyotajwa hapa juu. Kutafuta
na kutumia taarifa za masoko ya sehemu tofauti
Kwa kadri utakavyokuwa
unaendelea kuzalisha, mabadiliko mbali mbali yatatokea kuhusiana na uzalishaji
wako na hata kuhusiana na soko la bidhaa unayozalisha kwa maana ya kuku. Ili
uendane na mabadiliko yanayotokea ni muhimu mzalishaji upate taarifa za hali ya
soko mara kwa mara. Taarifa hizi zitakusaidia kufanya maamuzi yatakayokuwezesha
kuendelea kupata faida.
Taarifa za masoko
zinaweza kupatikna kwa wazalishaji kadhaa kuungana na kuunda umoja wao. Katika
umoja huo wawakilishi wachache wanakuwa na jukumu la kutafuta taarifa za masoko
ya kuku sehemu mbali mbali ambako kunaweza kuwapa wazalishaji tija zaidi. Walio
katika umoja huo watatumia taarifa hizo kufanya maamuzi ya kuuza kwa faida
zaidi kwa pamoja au kwa mmojammoja kutegemeana na hali halisi. Watoa taarifa
pia watafanya mawasiliano ya kuwajulisha wanunuzi juu ya upatikanaji wa kuku
kwenye maeneo wanakozalishiwa.
>>Mbinu zaidi ya kupata masoko mazuri
*Umoja wa kuzalisha na kuuza
Kwa kawaida kama bidhaa ina soko, wateja
hupatikana kwa urahisi pale wanapohakikishiwa upatikanaji wa bidhaa kwa wingi
katika sehemu moja. Katika hali hii, wanunuzi huwa tayari hata kununua kwa bei
ya juu zaidi kwa sababu ya kupunguza muda na gharama ya kutafuta bidhaa ya
kutosha kupeleka sokoni.a
Kwa upande wa kuku
jambo hili linawezekana kama mfugaji atafuga kuku wengi wa umri usiopishana
sana kwa wakati mmoja. Watakapofikia kimo kinachofaa kuuza utawauza wengi kwa
wakati mmoja na kwa faida zaidi. Mahali ambapo mfugaji mmoja mmoja hawezi
kukidhi wingi wa hitaji la wanunuzi, wafugaji kadhaa wanaweza kuunda umoja wao
wa kuzalisha (kila mmoja kwake ) na kuuza kwa kipindi kimoja na kupata faida
zilizotajwa hapa juu.
Faida nyingine ya kuuza
katika umoja ni kuongezeka kwa uwezo wenu wa kupanga na kusimamia bei mnayotaka
kuuzia. Sauti na uamuzi wenu wa pamoja utawapa nguvu ya kusimamia bei yenu
mnayoipanga dhidi ya bei za chini wanazotaka wanunuzi. Uwezo wako wa kusimamia
bei unyoitaka ni mdogo ukiuza peke yako.
Badilishana uzoefu nasi kwa kutueleza unachokifanya, acha comment yako hapa chini.
Labels: UFUGAJI, UFUGAJI WA KUKU