Ufugaji Bora wa Kuku wa Kienyeji – Part 2








KUZALIANA NA KUTOTOLESHA

>>Uchaguzi wa Kuku bora
Ili upate kundi lenye kuku bora huna budi uchague jogoo bora na matetea bora wa kuzalisha kundi lako.
Angalia sifa zifuatazo unapochagua:
i. Tetea na jogoo wawe na umbo kubwa.
ii. Wanaokua haraka.
iii. Wenye uwezo wa kustahimili magonjwa.
iv. Matetea wanaoweza kutaga mayai mengi
v. Matetea wanaweza kuatamia na hatimaye kutotoa vifarangakwa wingi na kuvilea
vi. Jogoo unaowachagua kwa ajili ya matetea au makoo yako wasiwe na uhusiano wa damu.

Ukiishachagua wazazi wa kundi lako changanya jogoo na matetea kwa uwiano wa jogoo mmoja kwa matetea 10 hadi 12. Ukiwa na matetea 20 utahitaji kuwa na jogoo wawili.
Nchini kwetu zipo aina tofauti za kuku wa asili ambao wana sifa tofauti. Wafugaji wengi hufuga kutegemeana na uwezo wa kuku kuhimili magonjwa ,kuwa na uzito mkubwa, utagaji wa mayai mengi n.k. Koo za kuku wa asili wenye sifa za namna hii ni aina ya Bukini , Kuchi, Kuchere na wa Kawaida wasio na ukoo maalum. Hawa kwa ujumla wao wakitunzwa vizuri wana uwezo wa kufanya vyema katika mazingira ya ya nchi hii kwa sababu wameishayazoea.

Soma: Kanuni za ufugaji bora wa kuku


>>Kuatamia na kuangua mayai:
Baada ya jogoo kupanda matetea au makoo, hawa watataga mayai. Mayai yanaweza kutotoleshwa kwa njia ya asili au kwa kutumia vifaa vya kutotolesha.

>>Kutotoa kwa njia ya asili
Hii inafanyika kwa kuku kuatamia mayai kwa hatua zifuatazo.

>>>Kuandaa kiota
         Kiota kiandaliwe kabla kuku hajaanza kutaga kwa kukiwekea nyasi kavu na kuzisambaza kwa kutengeneza muundo wa kata au sahani iliyozama kidogo.

Ufugaji-wa-kuku-wa-kienyeji
Kiota cha kuku

  Kiota kinyunyiziwe dawa ya unga kuua wadudu kabla na baada ya kuweka nyasi. Iwapo kuku atajiandalia kiota chake mahali panapofaa aachwe hapo ila kiota kiwekewe dawa ya kudhibiti wadudu.

Maandalizi ya kuku anayetaka kuatamia
Dalili za kuku anayetaka kuatamia ni:
  o    Anatoa sauti ya kuatamia.
o    Ushungi wake umesinyaa.
o Hapendi kuondoka kwenye kiota.
o Hupenda kujikusanyia mayai mengi

Kuku wenye dalili za kutaka kuanza kuatamia akaguliwe ili kuhakikisha kuwa hawana wadudu kama utitiri, chawa, viroboto n.k. wanaoweza kumsumbua wakati wa kuatamia. Akiwa na wadudu watamsumbua hataweza kutulia kwenye kiota na kuatamia vizuri. Matokeo yake ataangua vifaranga wachache. Hivyo walio na wadudu wanyunyizie dawa ya unga kabla hawajaanza kuatamia ili kudhibiti tatizo hili.

>>Kuatamia
Kuku anapotaga mayai yaondolewe na kubakiza moja kwenye kiota ili kumwita kuku kuendelea kutaga. Kuku akiwa tayari kuatamia awekewe mayai kwa kuatamia. Kwa kawaida kuku mmoja anaweza kuatamia vizuri mayai 10 hadi 13 kwa wakati mmoja.
Kipindi cha kuangua mayai ni kuanzia siku 20 baada ya kuatamia. Ukitaka kutotolesha vifaranga wengi kwa wakati mmoja, kuku akianza kutaga yakusaye mayai yake na kumbakizia yai moja ili aendelee kutaga.Mayai utakayokusanya yaweke mahali pasipo na mwanga mwingi na penye ubaridi kiasi.

Fanya hivi kwa kuku kadhaa wanaotaga ndani ya muda unaokaribiana. Kila atakayeonyesha dalili ya kuanza kuatamia muwekee mayai kati ya 10 na 12 aatamie. Kwa njia hii wataatamia na kuangua ndani ya kipindi kimoja. Na utapata vifaranga wengi wa umri mmoja hatimaye kuuza kuku wengi kwa pamoja.

Soma: Magonjwa ya kuku


>>Kulea Vifaranga
Baada ya vifaranga kutotolewa waache na mama yao mahali penye usalama kwa muda wa mwezi moja mbali na mwewe, vicheche, paka, kenge, n.k. Hakikisha wanapata maji na chakula cha kutosha muda wote.

>>>Kulea vifaranga kwa kumtumia kuku
Njia nyingine ni kuwaweka vifaranga mahali pazuri na kuwafunika na tenga ili kuzuia mwewe wakati wa mchana kwa kuhakikisha kuwa hawapigwi na jua wala kunyeshewa mvua.Wakati wa usiku warejeshe kwa mama yao ili awakinge na baridi. Fanya hivi hadi wafikie umri wa mwezi mmoja ndipo uwatenge na mama yao.

>>>Pia unaweza kutumia kifaa maalum cha kulelea vifaranga (kitalu/brooder) mara baada ya kuanguliwa. Katika kitalu wanapatiwa joto wanalohitaji. Kifaa hiki kinaweza kutengenezwakwa karatasi ngumu itumikayo kutengeza dari.

Au
Katika mazingira ya kijijini unaweza kutengeneza wigo wa mduara kwa magunia. Upana wake uwiane na wingi wa vifaranga ulionao na kina chake kama mita moja. Ukuta wake uwe na tabaka mbili za magunia hayo zilizoachana kwa nafasi ya inchi tatu au nne. Kati kati ya nafasi hiyo jaza maranda ya mbao au pumba za mpunga. Tayari utakuwa umepata kitalu cha kulelea vifaranga.

Ndani ya kitalu weka taa ya chemli ya kutoa joto linalohitajika kwa vifaranga. Fuatilia tabia ya vifaranga wanapokuwa katika kitalu.

Wakiisogelea sana taa ina maana joto halitoshi, ongezea joto kwa kupandisha utambi. Wakienda mbali sana na taa, joto limezidi punguza. Kitalu kikiwa na joto zuri vifaranga watatawanyika kote katika kitalu na kuonyesha kuchangamka.
Mama yao akitengwa na vifaranga arudishwe kwenye kundi lenye jogoo, atapandwa na kurudia kutaga mapema. Kwa njia hii kundi la kuku litakuwa kubwa kwa muda mfupi. Kwa kawaida vifaranga wengi hufa kabla ya kufikisha miezi miwili kutokana na baridi, kuliwa na wanyama wengine na magonjwa.

Ili kudhibiti magonjwa, vifaranga wapewe chanjo dhidi ya magonjwa yafuatayo:
a. Kideri ( New castle) siku ya 3 baada ya kuanguliwa, rudia baada ya wiki tatu kisha uchanje kila baada ya miezi mitatu.
b.  Kuhara damu au rangi ya ugoro (Coccidiosis) : Wapewe kinga kwa dawa ya Amprolium kwa siku 3 mfululizo wanapofikisha umri wasiku 7 baada ya kuanguliwa.
c. Gumboro wanashusha mbawa na kujikusanya pamoja kwa baridi, pia wanaharisha nyeupe.Hutokea kuanzia wiki ya 2 hadi ya 18.Wapewe chanjo siku ya 10 hadi ya 14 baada ya kuanguliwa na rudia baada ya siku 28 na 42. Kwa magonjwa mengine angalia maelekezo sehemu ya magonjwa ndani ya mwongozo huu.

Vifaranga wapewe chakula kilichoelezwa katika sehemu ya tatu ya kijitabu hiki na maji safi ya kutosha wakati wote kwa muda wa miezi miwili. Baada ya hapo wanapewa chakula cha kuku wanaokua.

Kuku wakikaribia kupevuka wakiwa na miezi mitatu hadi minne tenganisha temba na majogoo ili kudhibiti kuku wenye uhusiano wa damu wasipandane wao kwa wao. Wakipandana na mayai yao yakianguliwa hawatatoka vifaranga wenye sifa nzuri mfano: ukuaji wao utakuwa hafifu kuliko wazazi wao, uwezo mdogo kuhimili magonjwa na wengine wanaweza kuwa na ulemavu. Pia zingatia matemba hao wasipandwe na baba yao. Vilevile majogoo hao wasimpande mama yao.


UTUNZAJI WA KUKU

>>Ulishaji
Kuku kama mifugo mingine uhitaji chakula chenye virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini ili kukua upesi na kuwa na na afya nzuri . Chakula kinachofaa ni mchanganyiko wa viini lishe mbalimbali vyenye kazi tofauti mwilini. Kila kiini lishe hakina budi kiwe katika kiwango sahihi kulingana mahitaji ya mwili wa kuku katika umri tofauti.

Kuku anahitaji chakula chenye viini lishe vifuatavyo:

Kiini Lishe
Kinapatikana Katika Chakula Gani
Kazi Yake Mwilini

Wanga
Pumba,Chenga
za  nafaka
kama
Kutia nguvu mwilini

mahindi, mtama.







Mafuta
Mashudu yanayopatikana baada ya
Kutia
nguvu
na
joto

kukamua  mbegu  za  mafuta  kama
mwilini




alizeti, karanga n.k






Protini
Mashudu ya karanga au alizeti.Damu
Kujenga
mwili
na

iliyokaushwa  ya
wanyama
kama
kukarabati mwili


mbuzi, ng’ombe n.k. Mbegu za jamii






ya mikunde kama maharage, kunde,






soya....












Vitamini
Majani  mabichi  kama  mabaki  ya
Kulinda
mwili.
Majani

mboga za majani, michicha ya porini,
mabichi
pia
huwezesha

majani mabichi ya mipapai, majani ya
kuku kutaga mayai yenye

Lusina n.k.


kiina
cha  njano,
rangi




ambayo huwavutia walaji




wengi.




Madini (calsium
Unga wa dagaa,
unga wa
mifupa
Kujenga

mifupa,
na Fosforas)
iliyochomwa, chokaa

kutengeneza
maganda




ya mayai





Mfano wa kuandaa vyakula vya makundi tofauti ya kuku
Kwa Vifaranga
Kwa vifaranga vya tangu kutotolewa hadi miezi miwili tengeneza mchanganyiko ufuatao. Huu ni mfano mmojawapo wa kuandaa kilo 100 za chakula cha vifaranga. Iwapo utahitaji kuandaa jumla ya kilo 50 za chakula tumia nusu ya vipimo vilivyoainishwa katika jedwali hili.
Wastani wa mahitaji ya kuku wakubwa 50 kwa siku ni kilo 5. Chakula hiki ukigawe katika sehemu mbili na kuwapatia nusu asubuhi na nusu ya pili mchana.

Vifaa
Kiasi kwa kilo

Dagaa (unga au vichwa vya dagaa)
12 hadi 15

Chenga za nafaka kama mahindi au mtama n.k
40

Mashudu
20

Pumba
24

Chokaa
2

Unga wa Mifupa,Madini ( Premix)
2

Chumvi
Robo kilo

Mchanga
1

Jumla
Kilo 100




Kwa kuku wanaokua (baada ya miezi miwili ).





Vifaa
Kiasi kwa kilo

Dagaa (unga au vichwa vya dagaa)
7

Chenga za nafaka kama mahindi au mtama n.k
30

Mashudu
20

Pumba
39

Chokaa
2

Unga wa Mifupa,Madini ( Premix)
2

Chumvi
Robo kilo

Mchanga
1

Jumla
Kilo 100





Kama umeamua kufuga kuku kwa mtindo wa kuwaacha huru wajitafutie chakula (huria) unaweza kuwapatia vifaranga nyongeza ya protini.Utafanya hivyo kwa kuwachanganyia vumbi au vichwa vya dagaa kiasi cha kikombe kimoja vilivyotwangwa pamoja na pumba ya mahindi vikombe vitano.

>>Maji ya Kunywa
Mfugaji ahakikishe anawapatia kuku maji masafi ya kunywa na ya kutosha kila siku. Vyombo vya maji ya kunywa budi visafishwe vizuri kila siku. Hii itasaidia sana kudhibiti magonjwa yanayoweza kutokana na vimelea vya magonjwa vinavyostawi katika maji yasiyo safi. Kuku wanaweza kuwekewa maji katika aina tofauti ya vyombo kutegemea na urahisi wa kupatikana mfano sufuria, ndoo za plastik zilizokatwa kuruhusu kuku kunywa bila kuchafua.

>>Usafi katika banda
Matandazo yanayowekwa katika sakafu ya banda la kuku hayana budi yageuzwe mara kwa mara kwa wastani wa kila baada ya miezi miwili au mitatu . Wakati mwingine ni kabla ya kipindi hiki muda wowote yanapoloana na maji. Matandazo uharakisha kukauka kwa unyevu katika banda unaotokana na kinyesi cha kuku na pia zaidi na maji yanayomwagika.
Usafi katika banda utasaidia kudhibiti kwa kiasi kikubwa magonjwa mbalimbali.

>>Kuokota mayai
Usiyaache mayai ndani ya viota kwa muda mrefu, yaokote mara kwa mara ili kuepuka kuharibiwa kwa mayai hayo na kuku wenyewe. Kuku wanayo tabia ya kula mayai yao ikiwa chakula unachowapa kina upungufu wa protini.
Vilevile kiasi cha mwanga unaoingia ndani ya banda kikizidi kuku hula mayai au kudonoana wenyewe kwa wenyewe.Uonapo dalili za namna hii kwenye kundi lako punguza kiasi cha mwanga kwa kuziba sehemu za madirisha kwa vipande vya magunia au vipande vya makasha ya karatasi ngumu.

Kama ilivyoelezwa awali kuku wapewe majani mabichi ya kutosha mara kwa mara ili wawe wanakula hayo badala ya kudonoana.
Pia fuatilia kuhakikiksha kama chakula kina protini ya kutosha. Kama tatizo la kudonoana na kula mayai litaendelea omba msaada kwa mtaalam wa mifugo akuelekeze jinsi ya kuwakata au kuwachoma midomo.

Soma: Ufugaji Bora wa kuku - part 1


Labels: ,